• Jinsi ya Kupata Kibali cha Ujenzi



    Habari za wakati mpendwa msomaji! hivi kwa kawaida ni watu wangapi ambao wanafikiria kujenga? hapana shaka ukifanya utafiti utakuta kila binadamu mwenye akili timamu anafikiria kujenga. Hivyo basi twende pamoja katika habari hii muhimu kwako.


    Hatua za kufuata ili kupewa kibali cha kujenga jengo.
       Kwanza kabisa wanaotoa kibali cha kuruhusu jengo lijengwe  ni mamlaka za kiserikali za eneo husika hasa manispaa, kwa maana wao wanao ramani ya mji mzima inayoonesha mipangilio ya aina za majengo yanayotakiwa kujengwa katika kila mtaa.

    1. Hati halali ya eneo – Hii hasa kwa wale wanaotaka kujenga majengo ya gholofa na ya kibiashara ni lazima kuhakikisha unakuwa na hati halali inayoonesha kwamba sehemu unayotaka kujenga ni mali yako.

    mfano wa hati ya kiwanja
    2. Michoro kamili na iliyowekwa muhuri – hii ni ile ya msanifu majengo(architectural drawings) kwa majengo ya kawaida ya kuishi(residential) ya chini (one storey) kwa yale ya ghorofa pia itahitajika michoro ya mhandisi majengo(structural drawings), mhandisi umeme (electrical drawings), na michoro ya mfumo wa maji safi na taka (plumbing).

    mfano wa ramani ya muonekano wa jengo (3dimension)

     
    Kumbuka : michoro hii yote inatakiwa iwe imepigwa muhuri ili kuonesha kwamba imechorwa na wataalamu wenye sifa na wanaotambulika.
    kwa ushauri/maoni/swali wasiliana nasi kupitia
    email: omarisaidi77@gmail.com
    Namba ya simu: +255 753 629218, +255 689636501,
    Karibu Sana!!!
  • 0 comments:

    Post a Comment

    HAVE YOU RECOMMENDED TO USE GREAT PERSON?

    Yes, now here you are at the right place.Meet with innovative,creative and multi-purpose engineer.

    ADDRESS

    P.o.Box 5848,Tanga,
    TANZANIA

    EMAIL

    omarisaidi77@gmail.com

    TELEPHONE

    +25527 2646279

    MOBILE

    +255753629218
    +255689636501
    +255657781613