• JUA FAIDA ZA KUPAKA RANGI KATIKA KATIKA JENGO LAKO

    Image result for painting in building
    'Umuhimu wa kupaka nyumba rangi mpya'

    Kupaka rangi mpya kwenye nyumba au chumba kilichochoka ni dawa mojawapo ya kupendezesha makazi na kunaweza kukifanya au kuyafanya yawe maridadi zaidi
    Hivyo kama unataka kufanya nyumba yako iwe maridadi na ng’aring’ari tumia mbinu mbalimbali mojawapo ni kupaka rangi mpya na kuleta muonekano maridhawa.
    Kuchagua Rangi
    Ni muhimu kuchagua rangi kwa uangalifu. Ni vyema kuwatumia mafundi wanaofahamu zaidi jinsi ya kutengeneza ama kuchanganya rangi.
    Kumbuka kuwa zaidi ya kufanya nyumba yako ionekane maridadi, rangi pia inaweza kuathiri hali yako ya moyoni na utulivu wa akili. Rangi angavu husisimua akili na macho, lakini rangi ambayo si ya kung’aa huelekea kumtuliza mtu.
    Wataalamu wanasema huenda rangi fulani inaweza ising’are na kusababisha mdororo inapopakwa ndani ya kuta za jengo, lakini ikawa angavu zaidi inapopakwa nje ya jengo hilo. Kwa hiyo ni muhimu kujua rangi zinazofaa nje na ndani. Kupaka nyumba rangi ya njano ya dhahabu ‘gold yellow’ na “rangi nyeupe ya kijivu.” Kunaleta mvuto mwanana.

    Image result for painting in building
    Ni lazima kujua ni rangi gani unayopaswa kutumia kupaka nyumba hii ni kwa sababu zipo aina mbili za rangi ya nyumba nazo ni za mafuta na rangi za maji.

    • zile za mafuta huwa ngumu sana zinapokauka, kwa hiyo zinafaa zaidi mahali panaposhikwa au kuguswa guswa mara nyingi, kama vile kwenye milango na kwenye ncha za mbao.

    Hata hivyo, rangi za mafuta huchujuka na kutoka baada ya muda. 
    • Kwa upande mwingine, rangi za maji, huhifadhi rangi yake (hazipauki) na hazitoi harufu mbaya kama zilivyo za mafuta.

    Tofauti ya rangi ya maji na ya mafuta ni kwamba za mafuta zinasababisha joto zaidi lakini za maji zina nafuu. Kwa hiyo ni vyema zaidi wanaokaa kwenye majira ya joto kali wakaepuka za mafuta ni vyema kutumia za maji kwani ziko murua kwenye jua na baridi kali.

    Rangi zote mbili hung’aa kwa njia nne kuu na wataalamu husema aina ya kwanza ya mng’ao huitwa gloss inafaa kutumiwa katika vifaa ambavyo vinatumiwa sana .
    Aina ya pili inayoitwa satin inafaa kupakwa bafuni na mahali pa kupitia au mara kwa mara kwenye verenda . 
    Aina ya tatu inayoitwa low sheen 
    Na ya nne inayoitwa flat zinafaa chumba cha kupumzikia au sebuleni. Aina hiyo ya nne inafaa kutumiwa katika dari.

    JARIBU KUPAKA
    Related image

    Wakati mwingine ni vizuri kujifunza. Jaribu kupaka rangi na unapopaka rangi unatakiwa kuandaa mazingira ambayo hufanikisha kazi hiyo nayo ni pamoja na kuondoa fanicha au samani unatakiwa kutandika mashuka yaliyozeeka sakafuni ili kuzuia isianguke chini na kuacha madoa.

    Baada ya hapo unakwangua na kuondoa rangi ya zamani iliyochakaa inayokwanguliwa kutoka kwenye fremu za madirisha, ncha za mbao, na dari. Kama nyumba yako haijapakwa rangi hata siku moja na kuta zake zimepigwa plasta ziko katika hali nzuri, lakini zinahitaji kuoshwa kwa maji na sabuni kabla ya kupakwa rangi kwani zina vumbi.

    Kazi ya kupaka rangi inakereketa ni lazima kuvaa vichuja-hewa puani na midomoni? Ili kuzuia rangi na vumbi ya plasta isiingie na kusababisha kuwashwa koo.

    Ni vizuri pia kuvaa miwani ili kuzuia uchafu kuingia machoni wakati wa kufanya kazi. Ni vizuri kuwa waangalifu sana unapotumia rangi iliyotengenezwa kwa risasi.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    HAVE YOU RECOMMENDED TO USE GREAT PERSON?

    Yes, now here you are at the right place.Meet with innovative,creative and multi-purpose engineer.

    ADDRESS

    P.o.Box 5848,Tanga,
    TANZANIA

    EMAIL

    omarisaidi77@gmail.com

    TELEPHONE

    +25527 2646279

    MOBILE

    +255753629218
    +255689636501
    +255657781613