Omari Saidi

I am a Writer

Omari Saidi

Registered member of Enginners Registration Board(ERB) as Graduate Civil Engineer with 3+ years of experience.Capable in design,supervision and construction of any project.Committed in providing high quality services for any party of project focus on Quality,Cost and Time

  • P.o.Box 5848,Tanga City ,Tanzania.
  • +255753629218
  • +255689636501
  • +255657781613
  • omarisaidi77@gmail.com
  • www.manyanyagroup.tk
Me

My Professional Skills

i.Fluent use of AutoCAD, Civil3D, Masterseries and ArchiCAD.
ii.Excellence in Application of Microsoft Word, Excel, Power Point presentation .
iii.Computer maintenance,programming and IT skills.
iv.Excellent verbal and written communication skills, negotiating, supervisory and leadership skills.
v.Have a positive team oriented attitude and outstanding organization skills .



Building Costruction works 90%
Civil works 70%
Computer Maintenance 95%
Website and Apps Design 60%

Project management

Iam implementing construction projects in a guarantee of timely putting qualitatively executed structure within the budget.

Architecture

Creation of a unique concept, full architectural and engineering design of the objects for various applications, architectural is what experienced.

Electrician

A full range of services for the design and installation of electrical networks, the primary and backup power supply systems, lighting.

Modern design

I am unique when designing what you feel keeping constant cost and time.

construction services

Experience is about what makes me unique and special in construction category

Complete Engineering solution

The primary goal is to deliver the agreed scope safely, on schedule, on budget and with the highest possible quality. Our specialized professionals ensure clients are taken through their specific requirement step by step.

WHY I AM THE BEST FOR YOU!

I provide innovative and cost-effective constructional solutions. I build appliances, lighting, power systems and other products that help millions of homes, offices, factories and retail facilities around the world work better.

0
completed project
0
design award
0
SATISFIED CUSTOMERS
0
current projects
  • Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba



    cebookTwittGoogle+
    Nyumba Nzuri
    Nyumba ni hitaji muhimu kwa watu wote. Kila mmoja anatamani na ana ndoto za kununua au kujenga nyumba nzuri na ya kisasa. Ni kweli kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji rasilimali nyingi hasa fedha.
    Pamoja na gharama hizi za ujenzi wa nyumba bado watu wengi wamekuwa wakishindwa kupata nyumba nzuri huku wakiwa tayari wamepoteza kiasi kikubwa cha pesa. Ni wazi kuwa yapo makosa mbalimbali yanayosababisha hali hii yakiwemo yale ya ukosefu wa elimu pamoja na uzembe wa aina mbalimbali.
    Karibu ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu makosa 8 unayoweza kuyaepuka wakati wa kujenga nyumba ili hatimaye uwe na nyumba bora.

    1. Kutozingatia kanuni za kununua kiwanja

    Watu wengi hawafahamu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wanaponunua kiwanja. Hivyo hujikuta wakiingia katika matatizo mbalimbali kama vile kuvunjiwa nyumba zao, kujenga kwenye maeneo mabaya kama matindiga na mikondo ya maji. Ni muhimu kuhakikisha mambo yafuatayo kabla na wakati wa kutafuta kiwanja cha kujenga nyumba:
    • Kiwanja hakina umiliki zaidi ya mtu mmoja
    • Kiwanja hakina mgogoro wa kisheria
    • Kiwanja hakiko kwenye hifadhi ya barabara au mazingira
    • Kiwanja kinafaa kwa ujenzi (Siyo tindiga, eneo la magadi, eneo la maporomoko ya ardhi au mkondo wa maji)
    Ukizingatia haya utaweza kupata kiwanja kizuri kwa ajili ya kujenga nyumba bora kwa ajili ya matumizi yako.

    2. Uchaguzi duni wa ramani

    Mara nyingi mtu humwita fundi na kumwambia kuwa “nataka unijengee nyumba ya vyumba vitatu”. Fundi anapouliza ramani yako iko wapi wao husema we angalia tu nzuri alimradi iwe ya vyumba vitatu. Hili ni kosa kubwa sana kwani husababisha watu wengi kujengewa nyumba ambazo hawazipendi.
    Ramani nzuri kwa fundi inaweza isiwe nzuri kwako na familia yako. Zingatia uchaguzi wa ramani kwa makini kulingana na wewe unavyopenda, hili litakufanya pia upende nyumba itakayojengwa.




    Ramani
    Ramani mbaya.

    3. Kutokufanya makadirio sahihi

    Ni wazi kuwa umeona nyumba nyingi zikianzwa lakini hazimaliziki. Hili kwa kiasi kikubwa linatokana na kufanya makadirio na maandalizi duni kabla ya kuanza kujenga. Ujenzi wa nyumba unahitaji maandalizi mazuri hasa kifedha. Ni muhimu kujiandaa vyema kabla ya kuanza ujenzi ili usikwamie njiani.
    Mambo unayoweza kufanya:
    • Weka makadirio ya gharama za ujenzi ili angalau uandae kiasi fulani cha pesa.
    • Nunua baadhi ya vifaa kabla. Unaweza kununua mchanga, mawe, kokoto, nondo, mabati n.k. Ili kupunguza matumizi ya pesa wakati wa ujenzi.
    • Weka mipango ya kutunza mahitaji yako mengine ya pesa kabla ya kuanza ujenzi. Kwa mfano ada za shule, kodi mbalimbali, chakula n.k.
    • Punguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kabla na wakati wa ujenzi. Ikumbukwe kuwa pesa nyingi zitahitajika kwenye ujenzi.

    4. Kutokubainisha mahitaji

    Mahitaji ya nyumba hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Hivyo ni vyema ukabainisha mahitaji yako kwa nyumba husika. Nimeshuhudia watu wakijenga nyumba na kuzivunja ua kuzifanyia marekebisho kila mwaka kutokana na kutobainisha mahitaji yao mapema.
    Kurekebisha au kuvunja na kujenga upya nyumba yako kutakupotezea kiasi kikubwa sana cha pesa. Kwa mfano wengi hurekebisha nyumba zao ili kuongeza vitu kama vile jiko, choo na bafu, milango, madirisha n.k. ambavyo wangepanga mapema wangekuwa wameviweka mwanzoni.

    5. Kutokuwaza mbeleni

    Ni vyema kuwaza mbeleni kwani nyumba ni kitu utakachokitumia muda mrefu. Ni vyema ukafahamu vitu na mahitaji utakayoyataka kwenye nyumba yako kwa siku za mbeleni. Hili litakuwezesha kujenga nyumba utakayoitumia na kuifurahia kwa muda mrefu zaidi.
    Ni vyema pia ukawaza kuweka miundombinu ya kisasa kama vile umeme, simu (intercom), nyaya za televisheni, Kiyoyozi, na hata Data. Hata kama huna pesa za kuweka mambo haya unaweza kubuni nyumba ambayo baadaye itaruhusu miundombinu hii.




    Nyumba
    Nyumba ya Kisasa

    6. Kutumia mafundi duni

    Wengi hupenda kuokoa gharama kwa kutumia mafundi wenye uwezo mdogo ili wawalipe kwa bei nafuu. Ni wazi kuwa rahisi inaumiza. Jiande vyema kabla ya ujenzi ili uweze kuitendea haki nyumba yako kwa kutumia mafundi bora wanaoimudu kazi yao vyema. Kutumia mafundi bora kutakufanya kupata pia kazi yenye ubora.




    Nhazi
    Ngazi zilizokosewa.

    7. Kupuuza kanuni muhimu za ujenzi

    Ujenzi una kanuni zake mbalimbali ambazo ni vyema zikazingatiwa. Kutokana na uelewa mdogo, watu wengi hawazingatii kanuni muhimu za ujenzi kama vile kumwagilia maji yakutosha pamoja na kujenga nyumba kulingana na muda.
    Nimeshuhudia nyumba nyingi zikivunjika kutokana na kujengwa haraka haraka bila kutoa muda wa kutosha kwa nyumba kukomaa na kustahimili uzito. Pia nimeona watu wakipuuzia umuhimu wa kunyesha sehemu iliyojegwa kwa maji mengi; ni muhimu kunyesha vyema eneo lililojengwa kwani “uimara wa saruji ni maji”; unaweza kunyesha angalau kwa siku saba asubuhi na jioni.




    Nyumba iliyoporomoka
    Nyumba iliyoporomoka kutokana na kupuuza kanuni za ujenzi.

    8. Matumizi ya vifaa duni

    Kama nilivyoeleza katika maelezo yaliyotangulia, uhaba wa fedha huwafanya watu wengi kufanya kazi duni. Hivi leo kuna vifaa mbalimbali vya ujenzi, lakini si vyote ni bora. Kwa mfano, hakuna haja ya kununua kitasa kinachovunjika baada ya mwezi au vigae vinavyofubaa. Kwa kufanya hivi utapoteza pesa nyingi kwa kununua vifaa hivyo mara kwa mara. Jibane, jipange ufanye kitu cha uhakika.
    Hitimisho
    Ni wazi kuwa ujenzi wa nyumba ni shunguli pevu inayohitaji kutulia, moyo na maandalizi stahiki. Hakuna kitu kinachoshinda nia na mipango mizuri. Naamini kwa kuyaepuka makosa tajwa hapo juu utaweza kujenga nyumba bora, salama na ya kisasa kabisa.
    Je umeshajenga nyumba yako? Ulipata changamoto gani na ulizitatuaje? Au ndio unawaza usiku na mchana kuwa upate nyumba ya namna gani,Bei gani na kwamna gani?
    Tafadhali tushirikishe kwa kutoa maoni yako hapo chini. Pia unaweza kutupigia simu no.0753629218.
  • Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia ili Kupunguza Gharama za Ujenzi


    Nyumba
    Ikiwa unajenga nyumba mpya au unafanya ukarabati wa nyumba ya zamani, suala la kupunguza gharama za ujenzi ni muhimu sana.
    Watu wengi wamejikuta katika hali ngumu ya kifedha au hata kukwama katika ujenzi kutokana na kushindwa kuweka mikakati mizuri ya kupunguza gharama za ujenzi.
    Kwa kutambua umuhimu wa ujezi, na kwa kutambua kuwa ujenzi ni jambo linalogharimu fedha nyingi; nimeona ni vyema nikushirikishe mambo 10 muhimu unayoweza kuyazingatia ili uweze kupunguza gharama za ujenzi.

    1. Chagua kiwanja bora

    Uchaguzi sahihi wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi ni jambo muhimu sana. Watu wengi hujikuta wakitumbukia kwenye gharama kubwa za ujenzi kutokana na uchaguzi duni wa kiwanja.
    Hebufikiri ukinunua kiwanja sehemu ambayo ni mkondo wa maji au udongo wake unatitia; hili litakulazimu kutumia gharama kubwa zaidi ili kukifanya kiwanja hicho kifae kwa ujenzi, gharama ambazo zingeweza kuokolewa kama ungefanya uchaguzi sahihi wa kiwanja.

    2. Chagua ramani nzuri na rahisi

    Ni wazi kuwa watu wengi wanajenga nyumba kila kukikucha lakini siyo wote wanaojenga nyumba zenye ramani sahihi na bora.
    Pamoja na sababu kuwa suala hili linatokana na ukosefu wa elimu sahihi juu ya masuala ya ujenzi; ramani mbaya huwagharimu watu wengi fedha nyingi na mwishowe haziwapi nyumba walizozihitaji.
    Kwa mfano; ramani za nyumba za Ulaya (Hasa maeneo ya baridi) huwezi kuzijenga kwenye maeneo ya Afrika yenye joto. Inaweza kuwa ni ramani nzuri sana lakini ikawa na vitu vingi vinavyoongeza gharama zisizokuwa za msingi. Vivyo hivyo ramani ya rafiki yako inaweza isiwe bora kwako.
    Hivyo, hakikisha unachagua ramani nzuri na rahisi ambayo utaweza kuitekeleza vyema bila kukutengenezea mzigo mkubwa wa gharama.

    3. Fanya utafiti wa kutosha

    Kukurupuka na kuanza kufanya jambo ni suala baya sana. Utafiti katika suala la ujenzi ni jambo muhimu sana litakalokuwezesha kupunguza gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa.
    Unapaswa kutafiti yafuatayo:
    • Bei za bidhaa na vifaa vya ujenzi
    • Mafundi bora
    • Vifaa bora na vya bei nzuri
    • Teknolojia za kisasa kwenye ujenzi, n.k.
    Ukitafiti kwa kina masuala tajwa hapo juu pamoja na mengine yanayohusiana nayo, kwa hakika utapunguza gharama za ujenzi ambazo zingepotea kutokana na kutokuwa na uelewa sahihi.

    4. Tumia vifaa mbadala

    Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi, kumekuwepo na vifaa pamoja na malighafi mbalimbali ambazo zinarahisisha ujenzi, zinaokoa gharama za ujenzi pamoja na kulinda mazingira.
    Hivi leo zipo mbao maalumu, matofali au hata vifaa vya jamii ya vigae ambavyo vinaokoa gharama za ujenzi maradufu kuliko vifaa vya kawaida. Ikiwa utajikita kutumia vifaa hivi basi utaweza kupunguza gharama zisizo za lazima kwenye ujenzi.

    5. Simamia vyema manunuzi na ujenzi

    Watu wengi wamejikuta wakipoteza fedha nyingi sana kwenye miradi yao, hasa miradi ya ujenzi kutokana na kukosa usimamizi mzuri.
    Niimeona watu wakijenga nyumba kwa simu na kuishia kupata hasara kubwa. Fundi anakuambia leta mifuko 10 ya saruji kumbe ni minne tu inahitajika; fundi anakuambia ametumia kitu fulani kumbe ametumia kilicho dhaifu ili apate pesa yake ya mfukoni.
    Ni muhimu kuhakikisha unasimamia manunuzi vyema pamoja na ujenzi kwa ujumla na si kumkabidhi fundi kila kitu.

    6. Chagua msimu sahihi wa ujenzi

    Siyo kila majira yanafaa kwa ajili ya ujenzi; inakupasa kuchagua msimu sahihi unaofaa kwa ajili ya ujenzi.
    Ni wazi kuwa majira kama vile ya mvua nyingi siyo rafiki kwa ujenzi; hii ni kutokana na sababu ya changamoto za usafirishaji wa malighafi za ujenzi pamoja na changamoto ya mafundi kutokuweza kufanya kazi wakati mvua ikinyesha.
    Suala hili linaweza kutengeneza gharama za ziada ambazo hazikutarajiwa kama vile kuongezeka kwa gharama za usafirishaji pamoja na ununuzi wa vifaa kama vile turubai; gharama ambazo zingeweza kuepukwa ikiwa msimu wa ujenzi ungechaguliwa vyema.

    7. Tafuta fundi sahihi

    Hivi leo kuna mafundi wengi, lakini si wote ni mafundi bora. Kwa ajili ya kwenda kwa mazoea au kutokana na kukosa uelewa, watu wengi wamejikuta wakitumia mafundi ambao huwasababishia gharama kubwa za ujenzi.
    Hebu fikiri ukifanya kazi na fundi anayekosea kila kitu; ni wazi kuwa kazi itakuwa ni kujenga na kubomoa ili kurekebisha makosa.
    Suala hili litakusababishia kutumia pesa nyingi zaidi kwa ajili ya marekebisho; ilihali pesa hizo ungeziokoa kama ungechagua fundi bora.

    8. Fanya baadhi ya mambo wewe mwenyewe

    Ukiruhusu kufanya kila kitu kwenye ujenzi kwa kutegemea mtu anayehitaji malipo utajitengenezea gharama kubwa sana katika ujenzi wako.
    Kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya wewe mwenyewe au wanafamilia wako; mambo kama vile maandalizi ya awali ya kiwanja, kumwagilia maji sehemu iliyojengwa; kukusanya vipande vya mawe au tofali, n.k.
    Kwa kufanya mambo kama haya au hata zaidi kulingana na uwezo wako utapunguza sana gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa. Kumbuka! Linda tu usifanye kitu kinachohitaji ujuzi wa kitaalamu usiokuwa nao kwani kinaweza kuleta matatizo makubwa baadaye.

    9. Tumia tena malighafi

    Kuna kauli isemayo “mafundi ni waharibifu”; mara nyingi mafundi hupenda kutumia vitu hovyo hovyo bila kujali gharama yake.
    Mafundi watakata mbao mpya ili tu kupata kipande kidogo wanachokihitaji kuliko kuunga vipande viwili; wanaweza pia kuvunjavunja matofali au kukatakata mabati mapya ili kupata kipande  wanachotaka kuliko kutafuta kipande cha zamani kwa ajili ya eneo husika.
    Hivyo basi, ili kupunguza gharama za ujenzi, hakikisha unasimamia matumizi ya rasilimali zilizobaki au zilizokwisha kutumika. Vipande vya matofali, mabaki ya mawe, misumari ya zamani, au vipande vya bati vinaweza kutumika sehemu nyingine na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.

    10. Zingatia kanuni za ujenzi

    Kuna kanuni kadha wa kadha za ujenzi ambazo zisipozingatiwa zinaweza kusababisha hasara kubwa au ongezeko kubwa la gharama za ujenzi.
    Masuala kama vile unyeshaji wa sehemu iliyojengwa kwa saruji, uchanganyaji wa saruji, muda wa ujenzi, n.k. Ni baadhi tu ya mambo muhimu sana.
    Kwa mfano nyumba isiponyeshwa vizuri ni lazima itapata nyufa na itatengeneza gharama zaidi za marekebisho; kwa mfano pia nyumba ikilazamishwa kujengwa harakaharaka kuliko muda stahiki ni lazima itapata dosari mbalimbali ambazo zitagharimu fedha zaidi kuzirekebisha.
    Hivyo basi, ni muhimu sana kuzingatia kanuni zote za msingi za ujenzi ili kuokoa fedha ambazo zingepotea kutokana na kukiukwa kwa kanuni hizi.
    Hitimisho
    Yaliyoelezwa hapa juu ni mambo 10 muhimu unayoweza kuyafanya ili kupunguza au kuokoa gharama za ujenzi. Naamini kwa namna moja au nyingine umejifunza namna ambavyo unaweza kuokoa pesa nyingi amabazo zingepotea kwenye ujenzi bila ulazima wowote.
    Je, una swali au una maoni yoyote kuhusu sisi?  Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini 
  • Tambua Haya kabla ya ujenzi wa nyumba wako


  • id 2-Nyumba vyumba 4 ,2 Master Bedroom





  • id 1-Nyumba ya vyumba 4





    Ufafanuzi wa Kitaalamu wa Nyumba Hii

    Ukubwa wa Nyumba (SQM)187SQM
    Idadi ya Vyumba vya Kulala Vyote4
    Idadi ya Vyumba + Choo1
    Idadi ya Vyumba + Pakuvalia + Choo1
    Idadi ya Vyumba Kawaida2
    Idadi ya Dining1
    Idadi ya Sebule1
    Idadi ya Jiko1
    Idadi ya Stoo1
    Idadi ya Vyoo Public1
    Idadi ya Bafu Public1
    Idadi ya Veranda / Bakoni2
    Idadi ya Tofali za Block (6') kwa Kuta3367
    Idadi ya Tofali za Block (6') kwa Msingi1665
    Idadi ya Bati za Kawaida (mita 3 urefu)129
    Material ya Paa
    • Corrugated Iron Sheets
    • Industrial Trough
    • Clay Tiles
    Staili ya Paa
    • Pitch Roof
    Aina ya Kuta
    • Cement Sand Blocks
    Hali ya Hewa Inayofaa
    • Sunny
    • Windy
    • Rainfall
    Staili ya Nyumba  Classical
    Kiwango cha Gharama Ujenzi     A Bit Premium

  • HAVE YOU RECOMMENDED TO USE GREAT PERSON?

    Yes, now here you are at the right place.Meet with innovative,creative and multi-purpose engineer.

    ADDRESS

    P.o.Box 5848,Tanga,
    TANZANIA

    EMAIL

    omarisaidi77@gmail.com

    TELEPHONE

    +25527 2646279

    MOBILE

    +255753629218
    +255689636501
    +255657781613