Jambo kubwa ambalo limekuwa
likisababisha tafakari kubwa wakati wa mipango ya ujenzi wa nyumba ni namna
ya kufanikisha gharama kubwa zinazohitajika, ambazo zinaogopesha wengi. Hizi
ni kuanzia
|
|
Katika ujenzi, gharama huangukia katika rasilimali watu na vitu hususani gharama za ufundi pamoja na nyenzo za ujenzi. |
|
Katika mazingira ya sasa ambayo teknolojia imeendelea zaidi, ujenzi wa nyumba umekuwa ni kitu kinachohitaji utaalamu mkubwa ili uweze kukidhi sheria na miongozo iliyopo. |
|
Miaka ya nyuma ilikuwa inawezekana kujenga nyumba kwa namna ambayo unataka mwenyewe na ingewezekana kuwa na gharama ndogo zaidi, lakini miaka ya sasa taratibu na sheria zimekuwa zikilazimu kwa namna moja ama nyingine kujenga nyumba yenye kiwango na ubora unaokubalika. |
|
"Ni muhimu kujenga nyumba ambayo
imekidhi viwango vya kitaalamu na kisheria kwa manufaa bora".
|
|
Watu wengi wamekuwa wakilalamika ughali wa gharama unaotokana na kujenga kwa kufuata taratibu za kitaalamu bila kujua sababu zinazozalisha gharama hizo. |
|
Zipo sababu nyingi za msingi
ambazo zinafanya suala la ujenzi liwe la gharama kubwa.
|
|
Sababu
mojawapo ni pamoja na usanifu
na mipango ya jinsi ya kufanya uamuzi wa namna jengo na mifumo yake yote
inavyopaswa kuwa ikiwamo mwonekano wake, miundombinu, umeme, maji, mandhari na
kila kitu kinacho husiana na nyumba.
|
|
Usanifu ni hatua ya kwanza na
ya msingi katika ujenzi na kwamba unapokosea katika hatua hiyo upo uwezekano
mkubwa wa kukosea hata mwisho wa ujenzi wa nyumba husika.
|
|
“Ni muhimu kupata wataalamu ambao wamebobea
katika kufanya kazi hii ya usanifu ili uweze kuweka msingi mzuri wa nyumba
yako.
Hatua hii huweza kuhusika pia katika kukadiria gharama ambazo nyumba
yako itagharimu pamoja na muda ambao utahitajika kukamilisha ujenzi wako”.
|
|
“Lakini pia ili kupunguza gharama za ujenzi
unapaswa kujenga nyumba unayoihitaji, hii inamaanisha kuwa kuna watu
wanajenga nyumba ambazo hawazihitaji au hazitawasidia kwa muda ambao
wamekusudia. Kujenga nyumba ambayo ni kubwa mno au ndogo sana ni sawa na
kujenga nyumba ambayo huihitaji.
|
|
Hakikisha umeshirikiana na
mtaalamu wako kujadiliana katika mahitaji uliyonayo na dukuduku nyingine
unazozipenda ili uwe umeridhika na nyumba ambayo utaijenga.”
|
|
Tunashauri kutumia vizuri
kila nafasi iliyopo katika eneo ulilonalo wakati wa kujenga nyumba kwa sababu
ni mojawapo ya njia za kitaalam za kupunguza ghrama za ujenzi.
|
|
Pia kila ongezeko la eneo la
mita moja ya mraba katika nyumba inagharimu wastani wa Sh. 500,000 kwa nyumba
ya kawaida na kwamba hiyo inatoa picha halisi ya kuepuka kuwa na nyumba
inayochukua eneo kubwa bila sababu ya msingi.
|
|
|
|
|
|
|
|
Jambo jingine ambalo Tunashauri ni kuacha kuweka vitu visivyo vya lazima katika nyumba.
|
|
“Kwa mfano unaweza kuachana na madirisha ya
aluminiamu na ukatumia madirisha ya nyavu tu au ukaepuka kujenga makabati
vyumbani kwani yanaweza kuongeza gharama za matofali na saruji,”
|
|
Lakini pia achana na kujenga kila
kitu kwa tofali wakati mwingine kuacha nafasi kwa mfano kuwa na sebule, jiko
na sehemu ya kulia isiyotengwa na kuta kunaweza pia kusaidia kupunguza
gharama.
|
|
Zinapungua zaidi iwapo uezekaji
utapunguza matumizi makubwa ya mbao na mabati mengi bila sababu.
|

0 comments:
Post a Comment